Jeremiah 50:15-20


15 aPiga kelele dhidi yake kila upande!
Anajisalimisha, minara yake inaanguka,
kuta zake zimebomoka.
Kwa kuwa hiki ni kisasi cha Bwana,
mlipizeni kisasi;
mtendeeni kama alivyowatendea wengine.

16 bKatilieni mbali mpanzi kutoka Babeli,
pamoja na mvunaji na mundu wake akivuna.
Kwa sababu ya upanga wa mdhalimu
kila mmoja na arejee kwa watu wake mwenyewe,
kila mmoja na akimbilie
kwenye nchi yake mwenyewe.


17 c“Israeli ni kundi lililotawanyika
ambalo simba wamelifukuzia mbali.
Wa kwanza kumla alikuwa mfalme wa Ashuru,
wa mwisho kuponda mifupa yake
alikuwa Nebukadneza mfalme wa Babeli.”

18 dKwa hiyo hili ndilo Bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, asemalo: “Nitamwadhibu mfalme wa Babeli na nchi yake
kama nilivyomwadhibu mfalme wa Ashuru.

19 eLakini nitamrudisha Israeli katika malisho yake mwenyewe
naye atalisha huko Karmeli na Bashani;
njaa yake itashibishwa
juu ya vilima vya Efraimu na Gileadi.

20 fKatika siku hizo, wakati huo,”
asema Bwana,
“uchunguzi utafanyika kwa ajili ya kosa la Israeli,
lakini halitakuwepo,
kwa ajili ya dhambi za Yuda,
lakini haitapatikana hata moja,
kwa kuwa nitawasamehe
mabaki nitakaowaacha.

Copyright information for SwhKC